Msimu wa 17 wa Wiki ya Maonyesho na Tuzo za Mitindo za Swahili 2024 (Swahili Fashion Week and Awards), mojawapo ya majukwaa maarufu ya mitindo barani Afrika, unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba 2024, katika ukumbi wa Parthenon Hall/Greek Hellenic Club, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam. Tukio hili linalowakutanisha wabunifu zaidi ya 40, litasherehekea mtindo na ubunifu wa Kiafrika chini ya kauli mbiu: “Discover what makes Africa beautiful.”
Akizungumza kuhusu onesho hilo LA mitindo Mbunifu Mustafa Hassanali amesema Mwaka huu, maonyesho haya yataendana na kampeni ya “Nishati Safi ya Kupikia,” yakimuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama suluhisho endelevu na rafiki wa mazingira.
Tangu kuanzishwa mwaka 2008, Swahili Fashion Week imekuwa jukwaa muhimu kwa wabunifu kutoka nchi za Kiswahili na kwingineko, ikiwapa fursa ya kuonyesha kazi zao, kujitangaza kimataifa, na kukuza sekta ya mitindo ya Afrika.
Mwaka huu, tukio hili litatilia mkazo ubunifu wa kimazingira, likihamasisha matumizi ya malighafi rafiki wa mazingira na mbinu za uzalishaji wa kimaadili. Wabunifu wataonyesha miundo ya kipekee inayotilia maanani uendelevu, kwa kauli mbiu ya “Made in Africa.”
Mwanzilishi wa Swahili Fashion Week, Bw. Mustafa Hassanali, amesema
“Dhamira ni kuinua mitindo ya Kiafrika kwa viwango vya juu zaidi, tukithibitisha kuwa bidhaa za Kiafrika zinaweza kushindana kimataifa.”
Swahili Fashion Week and Awards inazidi kudhihirisha nafasi yake kama chombo cha maendeleo ya kijamii na kimazingira kupitia ubunifu wa mitindo
Mustafa anaongeza kuwa Swahili Fashion Week inalenga si tu kuonyesha mitindo, bali pia kuunda chapa za kimataifa zenye mizizi katika utamaduni na uendelevu wa Kiafrika. “Tunatarajia kuunda chapa zenye nguvu zinazoshindana na zile zinazoingizwa kutoka nje,” alisema Mwanzilishi, Mustafa Hassanal
Amesema Zaidi ya wabunifu 40 kutoka Tanzania na mataifa mengine wataonyesha kazi zao. Wabunifu wa ndani watajumuisha majina maarufu kama Sliq Shedafa, Kai Zuri by Sristi Bosco, Zawadi kutoka Zanzibar, na Jojo African Designs kutoka Dodoma. Pia, wabunifu wa kimataifa kama Dida (Italia), Iterik (Uganda), na Rheets Hanbok (Korea Kusini) watashiriki, wakiimarisha hadhi ya tukio hili
Hafla ya utoaji tuzo itatambua ubora katika vipengele 27. Mchakato wa kura za umma, utakaosimamiwa na Nexia Tanzania, utaweka uwazi katika kutambua vipaji bora.
Amewataja Wadhamini wakuu wa mwaka huu ni pamoja na Ubalozi wa Italia, Onomo Hotels, Coca-Cola, na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Pia, kuna ushirikiano wa kipekee na Camera Nazionale della Moda Italiana, unaowaleta wabunifu wa Italia kujifunza na kushirikiana na wenzao wa Kiafrika.
Swahili Fashion Week and Awards 2024 inasisitiza umuhimu wa mitindo katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, huku ikitangaza ubunifu wa Kiafrika kwa ulimwengu.