Bohari ya Dawa (MSD) imejinyakulia tuzo tatu za Mwajiri bora mwaka 2024 zinazotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Katika tuzo hizo zilizotolewa na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Biteko, MSD imeibuka na ushindi wa tuzo tatu ambazo ni pamoja na Taasisi bora kiutendaji (Club of Ten best performers), mshindi wa kwanza kwa taasisi inayotoa fursa za ajira (First runner up job creation na mshindi wa pili Mwajiri bora sekta ya umma (Second runner up Public Sector).