Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisaini kitabu cha Maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile nyumbani kwake Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Novemba, 2024. Dkt. Ndugulile alifariki dunia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimfariji mjane wa marehemu Dkt. Faustine Ndugulile, Dkt. Magdalena Lyimo wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Kigamboni, Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Novemba, 2024. Dkt. Ndugulile alifariki dunia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimfariji Mama mzazi wa marehemu Dkt. Faustine Ndugulile, Bi. Martha Ndugulile wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Kigamboni, Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Novemba, 2024. Dkt. Ndugulile alifariki dunia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.