Kampuni ya Kisheria inayomsimamia Mfanyabiashara Sandaland the Only One ambaye ndie Mtengenezaji wa jezi za SIMBA imemtumia barua Meneja wa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ikidai fidia ya BILLION TATU kutokana na kauli za kumchafua Mteja wao na imepelekea kuathiri biashara zake.
Wanadai Kamwe alitoa maneno kuwa Viongozi wa Simba wamemsema sana Sandaland kuwa wanatukanwa kisa yeye na wakamsusia uzinduzi wa jezi ndio maana akaenda kufanyia dukani kwake.
Kwenye Demand Notice hiyo wanataka KAMWE afanye mambo yafuatayo:
1- Kulipa fidia ya 3,000,000,000
2- Kumwomba msamaha hadharani Sandaland kwa kumkashfu kuwa anazalisha jezi mbaya hazina ubora.
3- Anapaswa kuomba msamaha kwa Umma kupitia vyombo vya habari vile vile alivyotumia kuongea alichoongea.
4- Ana siku saba (7) za kufanya yote hayo nje na hapo hatua kali zaidi watazichukua.