Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiwa katika foleni ya kupiga Kura kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi, kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Novemba 27, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akipiga Kura ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi, Novemba 27, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akiweka Kura yake katika sanduku kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi, Novemba 27, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga Kura ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi, Novemba 27, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka Kura yake katika sanduka kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi, Novemba 27, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 27, 2024 ameshiriki katika zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa, Lindi Novemba 27, 2024.
Akizungumza baada ya kupiga kura ambapo aliongozana na Mkewe Marry Majaliwa, Waziri Mkuu amewapongeza wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuchangua viongozi katika uchaguzi huo unaofanyika nchi nzima.
“Wananchi wamejitokeza kwa wingi, tayari mimi na familia yangu tumepata nafasi ya kumchagua kiongozi ambaye tunaamini atatuletea maendeleo kwenye kijiji chetu”.