……….
Happy Lazaro, Arusha .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwani ni haki yao ya msingi kufanya hivyo .
Aidha Makonda ameungana na Watanzania wengine kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye kituo alichokuwa amejiandikishia cha Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama Kata ya Sekei Jijini Arusha.
Makonda akizungumza na wanahabari mara baada ya kupiga kura kituoni hapo amewasihi wananchi wa Mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye Uchaguzi huo kwani ndiyo sehemu pekee inayompa uhuru na mamlaka mwananchi mwenye sifa katika kuchagua na kuunda serikali aitakayo.
Aidha Makonda amewataka wananchi mara baada ya kupiga kura kuondoka vituoni na kuachana na jukumu la kutaka kulinda Kura kwani jukumu hilo kulingana na sheria na taratibu za uchaguzi huo linabebwa na Mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo muhimu kwa maendeleo ya Mitaa na Vijiji.
Aidha amesema kuwa , zoezi la kupiga kura ni zoezi muhimu sana katika nchi yetu na linawapa wananchi uhuru wa kushiriki uchaguzi wanaotaka .
“Nawaombeni wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kimsingi na kuwaahidi wananchi kuwa na amani kwani hakuna tishio la uvunjifu wa amani.”amesema .
Makonda ameongeza kuwa, wageni wakija Arusha ni fursa kubwa kwetu kwani wananchi wanapata fursa ya kuweza kufanya biashara mbalimbali sambamba na kutangaza biashara zao.
Hata hivyo amewataka wananchi wasikubali uchaguzi wa serikali za mitaa ukawagawanya au kuharibu amani na utulivu wa mkoa wa Arusha hivyo kuwataka wananchi hao kufuata hatua zote kwenye utulivu mkubwa