Na Prisca Pances
Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano wa Ulinzi (JDCC) kati ya India na Tanzania imekutana Jana Novemba 26,2024,huko Goa nchini India katika kikao cha tatu kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano.
Katika mkutano huo, pande hizo mbili zilijadili kukua kwa ushirikiano wa mafunzo na huduma kwa huduma, ushirikiano wa sekta ya bahari na ulinzi. Pia, walipitia maendeleo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya yale yaliyojadiliwa katika vikao vilivyopita vya JDCC na kuchunguza maeneo mapya ili kupanua zaidi ushirikiano wa ulinzi wa nchi hizo.
Ujumbe wa India, ukiongozwa na Katibu Mwenezi Shri Amitabh Prasad, ulijumuisha maofisa wakuu kutoka Wizara ya Ulinzi na Vikosi vya Wanajeshi.
Kamishna Mkuu wa India nchini Tanzania Shri Bishwadip Dey pia alihudhuria mkutano huo. Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu Meja Jenerali Fadhil Nondo.
Kama sehemu ya ziara hiyo, wajumbe wa Tanzania watatembelea kampuni ya Goa Shipyard Ltd ili kupata uzoefu wa moja kwa moja wa uwezo wa India katika maendeleo ya bandari na ujenzi wa meli.
Ujumbe huo pia umepangwa kutembelea kituo cha usafiri wa ndege za kijeshi cha India INS Hansa na Taasisi ya Kitaifa ya Hydrografia huko Goa.
India na Tanzania zina uhusiano mzuri wa kirafiki ambao unaimarishwa na kujenga uwezo na njia za kuendeleza ushirikiano. Nchi hizo mbili zina mpango wa miaka mitano ya ushirikiano wa kiulinzi.