Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara Yanga SC wameanza vibaya katika michezo ya Kimataifa ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2 -0 dhidi ya Al Hilal omdurman ya Sudan katika mchezo uliochezwa leo Novemba 26, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mabao ya Al Hilal omdurman yamefungwa na Mshambuliaji Adama Coulibaly dakikia ya 64 pamoja na Yasir Mozamil dakika ya 90 ya mchezo.
Yanga SC wapo kundi A pamoja na Tp Mazembe, Mc Alger pamoja na Al Hilal omdurman.