Ikiwa imebaki siku 01 kuelekea Uchanguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho Novemba 27, 2024 Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Novemba 26, 2024 limefanya doria za magari na miguu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Songwe ikiwemo Mji wa Tunduma Wilaya ya Momba, Isongole na Itumba Wilaya ya Ileje pamoja na Kata ya Vwawa na Mji Mdogo wa Mlowo Wilaya ya Mbozi ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ulinzi na usalama.
Akizungumza mara baada ya doria hiyo, Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholaus Livingstone amesema kuwa doria hiyo ni sehemu ya kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Mkoa wa Songwe na viunga vyake.
ACP Livingstone alisema kuwa, doria katika Vitongoji, Vijiji, Mitaa na Kata mbalimbali ndani ya Mkoa wa Songwe zinazofanywa na Jeshi hilo ni sehemu ya kujua changamoto za kiusalama zinazowakabili wananchi na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto hizo ili Mkoa wa Songwe uendelee kuwa salama.
ACP Livingstone amewataka wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato bila wasiwasi wowote kwani Jeshi lao la Polisi Mkoa wa Songwe lipo imara kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaendelea kuwepo.
Ikumbukwe kuwa magari haya ya doria na vitendea kazi vingine ni juhudi ya serikali ya awamu ya 06 ambayo imekuwa ikitoa vifaa hivyo kwa awamu awamu ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limekuwa likiendelea kufaidika na vifaa hivyo.GUZI WA SERIKALI ZA MITAA.