Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba 2024
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na abiria waliosafiri pamoja naye kwa kutumia usafiri wa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kigoma leo tarehe 26 Novemba 2024. Amewasihi wananchi waliojiandikisha kuchagua viongozi bora katika uchaguzi huo.