Watumishi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege WIlaya ya Musoma Mkoani Mara wameguswa na upendo wa Mkaguzi kata ya Kisangura Wilaya Serengeti kwa kitendo cha kutoa viti mwendo kwa wananchi wenye changamoto ya Miguu kitendo kilichopelekea kuungana nae kutoa viti mwendo kwa wananchi hao.
Mkaguzi wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Genuine Kimario amebainisha kuwa amefurahi kuona wananchi na taasisi mbalimbali zinaendelea kuguswa na kuunga mkono kwa kuwasaidia wananchi wenye changamoto katika kata hiyo.
Amesisitiza kuwa mbali na utu na ubinadamu katika kuwasaidia wananchi hao hata vitabu vya dini vinawaambia kuwasaidia wahitaji ili kupata baraka kutoka Kwa Mungu wao alisema kimario.
Vile vile amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kata hiyo ili kupambana na uuhalifu na kata hiyo kuwa salama.