Wananchi wa mitaa ya kata ya Lwanhima wametakiwa kuchagua wenyeviti wa serikali za mitaa wenye uwezo wa kutatua kero na changamoto zao badala ya kuchagua kwa ushabiki na sababu nyengine zisizo za msingi
Rai hiyo imetolewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Nyamagana Ndugu Yusuph Ludimo wakati wa muendelezo wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa katika viwanja vya mtaa wa Maliza kata ya Lwanhima ambapo amewataka wananchi hao kuchagua wagombea wa CCM kwa kuwa ndio wenye uwezo wa kuzitambua na kuzitatua kero na changamoto zinazowakabili
‘.. Ndugu zangu ilani inayotekelezwa mpaka sasa ni ya chama cha mapinduzi, Na wenyeviti hawa tunaokwenda kuwachagua watakuja kufanya kazi na madiwani wa CCM, Mbunge wa CCM na Rais wa CCM, Sasa tusikosee tukachagua watu wasio na ilani inayotekelezwa tutajicheleweshea maendeleo ..’ Alisema
Aidha Ndugu Ludimo amewataka Vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuwa huo ndio msingi wa maendeleo kwani Serikali za mitaa ni za wananachi moja kwa moja hivyo kuhakikisha wanagombea na wanachagua viongozi wazuri kutoka CCM
Kwa upande wake diwani wa viti Maalum Mhe Lucy Lishinu amefafanua kuwa CCM ndio chama pekee kinachotoa fursa sawa Kwa watu wote bila kujali tofauti zozote walizonazo hivyo kuwaomba kukichagua chama hicho badala ya kuchagua vyama vyengine vyenye ubaguzi na visivyojali utu wa watu
Mikutano ya nje na ndani ya kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ya kata ya Lwanhima imeongozwa na Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa CCM wilaya ya Nyamagana Mhe Witness Makale kwa kushirikiana na Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Mwanza Mhe Kabila Shitobelo