Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Veronica Nduva akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusu mkutano huo
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .WAKUU wa Nchi nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wanatarajia kukutana mkoani Arusha Novemba 29 kwa ajili ya kushiriki Vikao vya kawaida pamoja na kuongoza maandalizi ya Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Arusha Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Veronica Nduva amesema kuwa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanaenda sanjari na kutoa elimu kwa wananchi juu ya shughuli zinazofanywa na jumuiya hiyo.
“ratiba za Maadhimisho hayo ya Miaka 25 ya EAC yatafanyika Kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano AlCC Jijini Arusha.”amesema .
Aidha Nduva amefafanua kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kupambwa na Tamasha la Kitamaduni litakalojumuisha Washiriki kutoka nchi zote za EAC,huku Vikao mbalimbali vikijadili kuhusu Amani na Usalama kwa EAC pamoja na Changamoto na mafanikio ya Jumuiya hiyo.
Nduva ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini Tanzania, kwani suala hilo limekuwa Kivutio kikubwa cha mikutano ya Kimataifa kufanyika Mkoani Arusha na maeneo mengineyo na kuwawezesha wao kuendelea kutekeleza mipango yao bila shida yoyote.
Amesema kuwa ,kwa kipindi.cha miaka 25 jumuiya hiyo imekuwa na mafanikio makubwa sana ambayo wanaweza kjivunia ambapo kupitia maadhimisho hayo ni fursa kwa watanzania ili waweze kuzungumzia.changamoto mbalimbali zinazowakabili na nini cha kufanya kwa.siku za usoni .
Amesema kuwa ,kabla ya kufika kilele hicho watajadili pia swala la soko.la pamoja na shirikisho la kisiasa ,maswala ya ushuru unaozuia biashara zetu zisifanyike kwa uhuru .
“Katika kilele cha sherehe hizi Marais wataweza kuzungumza kwa pamoja na kueleza namna jumuiya inavyofanya kazi na kuendelea na shughuli zake sambamba na kuzungumza mada mbalimbali ikiwemo ukuzaji wa uchumi wa maendeleo endelevu .”amesema Nduva.