Wekundu wa Msimbazi Simba Sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya wenyeji Pamba Jiji Fc katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa leo Novemba 22, 2024 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Bao la Simba Sc limefungwa na Mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba kwa mkwaju wa penati dakika ya 23 kufuatia kuangushwa kwenye eneo la hatari na benki Mkenya wa Pamba Christopher Oruchum.
Kwa ushindi huo Simba Sc imefikisha pointi 28 katika michezo 11 huku akiendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Mabigwa watetezi Yanga Sc ambao wana mchezo mmoja mkononi.
Pamba Jiji baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi 12 wakiwa nafasi ya 15 kwenye ligi yenye timu 16 ambapo mwisho wa msimu timu mbili zinashuka daraja.