Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo tarehe 21/11/2024 wameendelea na zoezi la Elimu ya kodi mlango kwa mlango katika eneo la Tabata Chang’ombe Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam kwa lengo la kuelimisha wafanyabiashara juu ya mambo mbalimbali ya kodi sambamba na kusikiliza changamoto na maoni yao.