Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) limekabidhi Hundi ya shilingi milioni 20 katika kitengo cha maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ,ikiwa ni mchango wa kuwezesha shughuli za uokoaji katika Jengo la ghorofa lililoporomoka Kariakoo hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Akizungumza leo Novemba 21, 2024 Katika eneo la tukio kariakoo Jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Jenerali mstaafu George Waitara amesema kuwa tukio hilo limesababisha maafa makubwa ikiwemo vifo,uharibifu wa mali pamoja na matatizo ya kisaikolojia kwa waathirika wa tukio hilo.
” TANAPA ni sehemu ya wananchi wa Tanzania,hivyo tumeguswa tukaona tutoe chochote ili kusaidia zoezi la Uokoaji” amesema Jenerali Waitara.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratubu Dr.Jimmy Yonazi ameishukuru TANAPA kwa msaada huo,nakuwaomba Watanzania walioguswa na maafa hayo waendelee kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi la uokoaji kwa haraka.
Pia ametangaza “control Number ” kwa ajili ya wananchi ambao watakaoguswa kutuma michango yao kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji.
” Control number ni 987320001709 ambapo namba hii inatumika kwa mitandao yote ,mwananchi anaweza kuchangia kuanzia 1000 nakuendelea na fedha hizi zinaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya Maafa ambayo ni 9921159801″ amesema Dkt.Yonazi