Awali Balton Makweta ambae ni katibu wa CCM kata ya Kichiwa amesema haijawahi tokea makatibu kupewa vifaa hivyo kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao na huenda ikawa likawa ndiyo jimbo la Kwanza kuwa na makatibu wanaotumia Komputa zao kutekeleza majukumu.
Kwa upande wake Mario Kuchungula ambaye ni mwenyekiti wa makatibu jimbo la Lupembe amemshukuru mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm wilaya kwa kitendo cha kuguswa na changamoto zao za kutumia karamu kuandika taarifa kwa mkono na kisha kuamua kuwapa Kompyuta hivyo anakihakikishia chama chake kwamba kupitia vifaa hivyo vya TEHAMA wanakwenda kulifanya jimbo hilo kuwa la kwanza kitaifa kukipa ushindi chama cha mapinduzi.
Nae Beno Nyato ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya amesema kilichomsukuma kuwapa kompyuta makatibu wote wa jimbo la Lupembe ni kutokana na changamoto ya mabadiriko ya teknolojia yanayoendelea kutokea duniani na kwamba kupitia vifaa hivyo hakuta kuwa na utaratibu wa makatibu kufunga safari umbali mrefu kila siku kupeleka ripoti zao makao makuu na badala yake watatumia barua pepe kutuma taarifa wakiwa maeneo yao ya kazi
Aidha Nyato ametoa na Flashi kwa kila kata ili itumike kwa ajili ya shughuli za chama inapohitajika ili kuondokana na matumizi mengi ya karatasi zinazopelekwa kuchapwa stationari huku pia akisema ameamua kutoa Kompyuta za mezani kwa kata zenye umeme na Kompyuta mpakato kwa kata zisizo na umeme kwakuwa zina uwezo wa kutunza moto.
“Nimetoa kompyuta na flashi kwa kila katibu kata ili kumaliza changamoto ya makatibu kutembea na taarifa umbali na kujikuta wakipoteza madaftari ambayo yameandikwa taarifa za kata zao zinazohusu chama “alisema Beno Nyato Mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Njombe.