Na Mwamvua Mwinyi
Novemba 20,2024
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufanyabiashara kihalali na kulipa Kodi ya Serikali kwa wakati.
“Nawasihi sana,nipeni ushirikiano ili sote tukishirikiana tupate Mapato yatakayo hudumia wananchi. Tukiungana kukusanya Mapato,tunakwenda kuibadili Kibaha Kimaendeleo”amesema Dkt.Shemwelekwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon John ametoa vyeti Maalum kwa kampuni ya Admire na National oil kutambua wepesi wao wa kulipa Kodi kwa wakati.
Wawakilishi kwa niaba ya Wafanyabiashara Negero na Admire wamesema kuwa wamefurahishwa na utaratibu Mpya wa Mkurugenzi Dkt. Shemwelekwa kuwatambua na kuwaita kubadilishana naye uzoefu kibiashara na kwamba amelenga kuboresha biashara zao.