WANANCHI wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Biubwa Said Mbarak Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar,aliyekuwa muandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakielekea katika Msikiti Mabuu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya Sala ya Maiti iliyofanyikaleo 18-11-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Marehemu Biubwa Said Mbarak Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar, aliyekuwa Muandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) iliyoongozwa na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume, iliyofanyika katika Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024 na (kulia kwa Rais) Mume wa Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe.Khamis Yussuf Mussa na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Biubwa Said Mbarak aliyekuwa Muandishi wa Habari wa ZBC, ikisomwa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Othman Chum, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti, iliyofanyika katika Msikiti wa Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024 na (kulia kwa Rais) Mume wa Marehemu Mbunge wa Jimbo la Kwahani Zanzibar Mhe. Khamis Yussuf Mussa na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Biubwa Said Mbarak aliyekuwa muandishi wa Habari wa ZBC, baada ya kumalizika kwa Sala ya Maiti iliyofanyika Msikiti Mabuluu Mfereji wa Wima Wilaya ya Mjini Unguja leo 18-11-2024, na (kushoto kwa Rais) Baba mzazi wa marehemu Said Mbarak Suleiman.(Picha na Ikulu)
…….