Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Magufuli (wa pili kutoka kushoto) akizungumza jambo na muwasilisha mada Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa (wa kwanza kushoto) mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Aliyekaa kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi.
Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa akifanya wasilisho kuhusu Maslahi ya Taifa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa (hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Maslahi ya Taifa kwa watumishi hao walipokuwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala ya utendaji kazi.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
…….
Na. Mwandishi Wetu Novemba18, 2024
“Tambueni kuwa Utumishi wa Umma ni kazi ya Mungu, fanyeni uamuzi kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa na msiwe na jaziba, visasi wala upendeleo ili kulinda maslahi ya Taifa”
Wito huo umetolewa Novemba18, 2024 na Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Taaluma Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, Dkt. Juma Kanuwa wakati akifanya wasilisho kuhusu Maslahi ya Taifa kwa Watumishi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI Mtumba, Jijini Dodoma.
Ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni muhimu kwa ustawi wa Taifa la Tanzania kwa kuwa inasimamia rasilimaliwatu, hivyo, Watumishi wake wanatakiwa kufanya uamuzi wakati wote kwa
kuzingatia uadilifu, falisafa ya nchi, uwezo wa nchi kiuchumi, rasilimali zilizopo na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Amewasisitiza pia Watumishi kupendekeza jambo la maendeleo kwa kuzingatia miongozo na kufuata ngazi za madaraka, uzalendo na hatimaye viongozi waweze kufanya uamuzi kwa kwa kuzingatia ilani ya chama husika na Maslahi mpana ya taifa.
“Ni fahari kubwa kuitumikia nchi yako kwa umahiri na uwezo mkubwa na epuka kuwa na kinyongo unapotekeleza majukumu ya Kitaifa kwa kuwa maslahi ya taifa yanaanzia kwa mtu binafsi” Dkt. Kanuwa.
Akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala Bw. Musa Magufuli alimshukuru Dkt. Kanuwa kwa kutoa elimu hiyo kwa watumishi wake na ameahidi kuchukua wasilisho
hilo na kulisambaza kwa watumishi wote ili waendelee kujifunza ingawa haitaondoa dhana ya kuita wawezeshaji kutoa elimu hiyo.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na Ofisi hiyo wa kutoa uelewa kuhusu masuala mbalimbali katika Utumishi wa Umma ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.