Watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara wamekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni njia ya kutatua changamoto ya usafiri iliyokua ikiwakabili watendaji hao hasa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mlimba uliopo Halmashauri ya Mji Ifakara.
Pikipiki hizo zilinunuliwa mara baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi . Zahara Michuzi kukataa kununuliwa gari kutoka kwenye Fedha za mapato ya ndani kiasi cha Shilingi Milioni 186,000,0000 zilizokua zimetengwa kwaajili ya Ununuzi wa Gari la Mkurugenzi, Hivyo badala akaomba fedha hizo zielekezwe kwenye matumizi ya ununuzi wa Pikipiki za watendaji wa Kata 19 za Halmashauri ya Mji Ifakara, na kiasi kinachobakia kielezwe kwenye shughuli nyingine za miradi mbali mbali ya Maendeleo.
Hivyo kupitia Vikao mbalimbali vya kisheria vya Halmashauri, CMT na Madiwani wa Halmashauri ya Mji