……..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuongoza timu ya kukagua majengo yote ya Kariakoo ili kupaa taarifa kamili ya hali ya majengo baada ya kumaliza zoezi la uokoaji.
Akizugumza na watanzania kupitia vyombo vya habari leo Novemba 17, 2024 kuhusu tukio la kuporomoka kwa jengo la gorofa katika soko la Kariakoo, Dar es Salaam Rais Mhe. Samia, amesema kuwa baada ya zoezi la uokozi kukamilika waziri Mkuu ataongoza timu ya wakaguzi wa majengo katika soko hilo.
Rais Mhe. Samia amesema kuwa Serikali itaweka wazi kuhusu taarifa ya uchunguzi baada ya kupatikana pamoja na kuchukua hatua ambazo serikili zitaeleza kwa kina.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa kariakoo, kufatia tukio hilo amepata taarifa za mara kwa mara kutoka kwa Waziri Mkuu kuhusu mwenendo wa uokoaji na unavyoendelea” amesema Rais Mhe. Samia
Rais Mhe. Samia amesema kuwa mpaka ufikia leo majira ya saa 4 asubuhi watu 84 wameokolewa na kufikishwa katika hospitali kwa ajili ya matibabu, huku majeruhi 26 wanaendelea na matibabu.
Amebainisha kuwa mpaka sasa watu 13 wamepoteza maisha katika tukio hilo, huku akieleza kuwa serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruliwa pamoja na kuhakikisha waliofariki wanastiliwa vizuri.
“Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili, niwaombe watanzania wote tuwaweke wote katika maombi walioathirika na tukio hili, tuwaombee pumziko la amani wote waliopumzika mbele ya haki” amesema Rais Mhe. Samia.
Rais Mhe. Samia amesema kuwa mpaka sasa hakuna sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka kutokana kwa kipindi hiki nipaombele chao kuwaokoa watu waliokuwa ndani ya jengo.
“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu zoezi la uokozi hadi litakapo kamilika, tunavipongeza na kuvishukuru vyombo vyote vya usalama vinavyoendelea na zoezi la ukoaji wa ndugu zetu pamoja na Mashiriki binafsi waliojitolea na kutoa ushirikiano” amesema Rais Mhe. Samia.