Na Prisca Pances
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Daniel Sillo amelitaka Jeshi la Magereza kuongeza ushirikiano wa ndani na nje ya nchi ilikukabiliana na mabadaliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia katika kupambana na uhalifu.
Awali Sillo amewataka wahitimu kutumia maarifa waliyoyapata kwa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na sheria ,kutunza na kusimamia wafungwa waliopo gerezani katika vituo vyao vya kazi.
Sillo amesema hayo Leo Novemba15,2024 wakati wa mahafali ya pili ya Stashahada ya Sayansi na Urekebishaji yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma cha Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga Dar es salaam.
“Ninyi nyote ni mashahidi kuwa mabadaliko ya teknolojia yamesababisha ongezeko kubwa la uharifu katika jamii zetu hivyo maarifa mliyoyapata yakawasaidie katika kupambana na watu hawa ,”amesema.
Pia amewahasa wahitimu kutoa elimu kwa wafungwa iliwanapomaliza vifungo vyao na kurudi kwenye jamii wawe raia wema na wajikita zaidi katika uzalilishaji ili kuepuka kurudia makosa.
Amesema wizara itafanyia kazi maombi yote yaliyowasilishwa ilikuendelea kuboresha miundo mbinu ya elimu na magereza kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kushauri wizara kutenga bajeti ya kuboresha miundo mbinu
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amemuomba naibu waziri kupitia wizara yake kujenga hospitali ya wilaya katika gereza hilo kwa ajili ya kuhudumia wafungwa askari pamoja na wananchi wa maeneo hayo.
“Chuo hiki kina kituo cha Afya chenye vifaa tiba na wahudumu wazuri lakini ombi letu kwako tunaomba tupewe hospitali kubwa itakayohudumia watu wengi zaidi kwani eneo tunalo,”amesema Mpogolo.
Katika mahafali hayo wahitimu 47 katika mwaka wa masomo 2023/2024 wametunukiwa shahada kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.