Mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru, umefika katika makaburi ya Kondo, Kinondoni, kwa ajili ya mazishi. Shughuli hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete viongozi wa serikali, ndugu, jamaa, na marafiki waliokuja kumpa heshima za mwisho.
Marehemu anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kusimamia mipango ya maendeleo ya taifa na mchango wake katika sekta ya fedha na uchumi wa nchi.
Mazishi yamefanyika kwa heshima kubwa, yakifuatana na maombi maalum kwa mujibu wa taratibu za kidini. Wakati wa shughuli hizo, hotuba mbalimbali za kumbukumbu zilitolewa na watu waliomfahamu marehemu, wakimtaja kuwa kiongozi aliyekuwa na maono na mchango mkubwa kwa taifa.
Familia ya marehemu imeeleza shukrani kwa wote waliojitokeza kuwafariji na kushiriki katika mazishi hayo. Tunawatakia faraja katika kipindi hiki cha majonzi.
Mwili wa marehemu Lawrence Mafuru ukiwasili katika makaburi ya Kondo Ununio jijini Dar es Salaam kwa mazishi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mawaziri, pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa katika mazishi hayo.
Mke wa Marehemu na watoto wa marehemu wakiwa katika mazishi hayo.
Mwili wa marehemumarehemu Lawrence Mafuru ukishushwa katika kaburi kwa ajili ya kupumzishwa