*Utazalisha tani 219 za Chuma.
*Tani 175,400 za Titanium
*Tani 5000 za Vanadium
*Tanzania*
Wakati Serikali ikiendelea na jitihada mbalimbali za kutafuta mwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,Tanzania inatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya chuma Barani Afrika.
Wakati jitihada hizo zikiendelea mnamo Agosti 3 , 2024 Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilitia saini makubaliano ya uchimbaji wa makaa ya mawe na chuma katika mradi wa Maganga Matitu na kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania Co.Ltd itakayowekeza kiasi cha Dola za Marekani milioni 77.
Ikumbukwe kwamba hivi karibuni ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt.Samia Suluhu Hassan aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara , Mipango na Uwekezaji kukamilisha mchakato wa kupata kampuni itakayowezesha kuanza kwa mradi wa Liganga na Mchuchuma.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa mradi wa Liganga na Mchuchuma ukikamilika utazalisha kiasi cha tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70, na madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni pamoja na Titanium tani 175,400 kwa mwaka na madini aina ya Vanadium tani 5000 kwa mwaka.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 , uanzishwaji wa kiwanda cha kuchenjua chuma na bidhaa zitokanazo na chuma.