Na Ashrack Miraji Fullshangwe Media
Bunju Beach Veteran wameahidi kuendelea kuhamasisha na kushiriki katika Tamasha la Same Utalii Festival tarehe 20 hadi 22/12/2024 lenye lengo la kuibua vivutio vya Utalii na kukuza uchumi wa Wilaya ya Same.
Viongozi wa Bunju Beach Veteran wametoa kauli hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same walipofika kumshukuru Mkuu wa Wilaya Kasilda Mgeni Kwa mapokezi na ushirikiano walioupata wakiwa Wilayani same kushiriki Mechi ya kirafiki kati yao na Same Veterani pamoja na kushiriki tukio la usafi wa mazingira katika mji wa Same.
Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya katika tukio hilo, Katibu tawala Upendo Wella amewapongeza Veteran hao kwa ushirikiano wao waliouonesha kushiriki katika shughuli za kijamii pamoja na kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya za kuitangaza Same kupitia Utalii.
Aidha amewataka kushiriki vyema kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi bora siku ya Tarehe 27/11/2024.
Kwa upande wao Viongozi wa Same Veteran wamesema wako tayari wakati wote kushirikiana na Mkuu wa Wilaya kuhakikisha uchumi wa Same unakuwa na watu wanakuwa na Afya bora kupitia Michezo.