Mratibu wa Mradi wa Khune Profesa Omary Swalehe (kulia) akimkabidhi Cheti cha mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji Afisa Manunuzi Mkuu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Melkiory Sellema (kushoto) baada ya kushiriki mafunzo ya siku tatu yaliofanyika kuanzia Novemba 6-8, 2024 katika Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA).
Mratibu wa Mradi wa Khune Profesa Omary Swalehe akizungumza jambo wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji yaliofanyika kwa siku tatu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Ndaki ya Dar es Salaam.
Meneja wa Mradi wa Khune Foundation Bi. Florah Michae akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji yaliofanyika kwa siku tatu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Ndaki ya Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya ununuzi, ugavi na usafirishaji kutoka sekta binafsi na watumishi wa umma wakipokea vyeti kutoka kwa Mratibu wa Mradi wa Khune Profesa Omary Swalehe baada ya kuitimu mafunzo hayo.
Mkufunzi Mwandamizi wa Mafunzo ya Ugavi, Ununuzi na Usafirishaji Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu ya Morogoro Mhadhiri Dkt. Paul Nsimbila
akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa ununuzi, ugavi na usafirishaji yaliofanyika kwa siku tatu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Ndaki ya Dar es Salaam.
………..
Zaidi ya Wataalamu 65 wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji kutoka sekta binafsi na watumishi wa umma wamejengewa uwezo na Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Khune Foundation kuhusu usimamizi wa mikataba kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi jambo ambalo litawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.
Akizungumza Novemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji, Mratibu wa Mradi wa Khune Profesa Omary Swalehe, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kujifunza ili waweze kufanya vizuri katika utendaji wao wa kazi.
Profesa Swalehe amewapongeza wataalamu wa ununuzi, ugavi na usafirishaji kwa kufanikiwa kushiriki mafunzo ambayo yana umuhimu mkubwa katika kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.
“Nawasihi tunapoanda semina nyingine mshiriki kwa wingi ili kuongeza maarifa yatakayowasidia kufanya vizuri katika utendaji wa kazi” amesema Profesa Swalehe.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa elimu waliyopata kwa muda wa siku tatu katika Chuo Kikuu Mzumbe inakwenda kuwasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi.
Afisa Manunuzi Mkuu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Melkiory Sellema, amesema kwa muda wa siku tatu wamepata elimu ya usimamizi wa mikataba kwenye mnyororo wa manunuzi ikiwemo namna mikataba ya manunuzi inavyotengenezwa.
“Tumejua namna ya kusimamia mikataba ya ununuzi kuanzia hatua ya awali hadi mwisho pamoja na kutatua migogoro kama ikitokea baina ya mtoa huduma na mpokea huduma” amesema Bw. Sellema.
Bw. Sellema amekishukuru Chuo Kikuu Mzumbe na Khune Foundation kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani yanakwenda kupeleka uweledi mpya katika taasisi zao katika suala nzima la manunuzi pamoja na ushiriki mzuri kwa kuzingatia sheria za manunuzi zilizopo.
Afisa Manunuzi Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Morogoro Bi. Eva Sichome, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo amefanikiwa kuongeza ujunzi katika usimamia mikataba pamoja na namna bora ya kuandaa mikataba.
“Tumejifunza namna ya kutengeneza mahusiano mazuri bila kuweka mianya ya rushwa na tamaa katika utendaji wa kazi yetu ili tuweze kufika thamani ya fedha ya miradi ya taasisi na Taifa kwa ujumla” amesema Bi. Sichome.
Hatua ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji umekuja baada ya kubaini changamoto katika taarifa mbalimbali ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PPRA) katika eneo la usimamizi wa miktaba hali sio nzuri kwani fedha nyingi zinapotea kutokana na wasimamizi kutokuwa na uwelewa mkubwa.
Chuo Kikuu Mzumbe kimedhamiria kuendelea kutoa mafunzo kwa wataalam wa ugavi, ununuzi na usafirishaji katika nyanja mbalimbali ili kuhakikisha kunakuwa na ubora na ufanisi katika sekta hiyo.