Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Mrisho Malipula akizungumza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wataalam wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji yaliyofanyika Novemba 7, 2024, Dar es Salaam.
Mwakilisha wa Mratibu wa Mradi wa Kuhne Foundation kwa Tanzania, Bi. Grace Nifasha Rusasa, ambaye ni Data Meneja wa Khune Foundation akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wataalam wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji yaliyofanyika Novemba 7, 2024, Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Mafunzo ya Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu ya Morogoro Mhadhir Dkt. Paul Nsimbiwa Kabelele akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wataalam wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji yaliyofanyika Novemba 7, 2024, Dar es Salaam.
Washiriki wakiwa katika mafunzo.
Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Mhadhiri wa Chuo hicho Dkt. Mrisho Malipula
………
Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Khune Foundation imewajengea uwezo Wataalamu wa Ununuzi, Ugavi na Usafirishaji kutoka sekta binafsi pamoja na watumishi wa umma kuhusu usimamizi wa mikataba kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi.
Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini changamoto katika taarifa mbalimbali ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi na Ugavi (PPRA) katika eneo la usimamizi wa miktaba hali sio nzuri kwani fedha nyingi zinapotea kutokana na wasimamizi kutokuwa na uwelewa mkubwa.
Akizungumza leo Novemba 7, 2024 Jijijni Dar es Salaam kwa niaba ya Rasi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mhadhiri wa Chuo hicho Dkt. Mrisho Malipula wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tatu kwa wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi 65, amesema kuwa ununuzi na ugavi ni eneo muhimu katika uendeshaji wa Taifa lolote.
Dkt. Malipula amesema kuwa katika bajeti nchi, serikali imekua ikitumia fedha nyingi katika ununuzi, ugavi na usafirishaji ili kuhakikisha jamii inapata huduma stahiki.
“Tukishindwa kufanya vizuri katika eneo la ugavi na ununuzi kutakuwa na matokeo mabaya katika Taifa letu pamoja na watu wake. Hivyo, semina hii itawasaidia watu wa ununuzi na ugavi katika kuhakikisha wanakwenda kutekeleza majukumu kwa ufanisi “amesema Dkt. Malipula.
Akimuwakilisha mratibu wa mradi wa Kuhne Foundation kwa Tanzania, Bi. Grace Nifasha Rusasa, ambaye ni Data meneja wa Khune Foundation, amesema kuwa
lengo la kudhamini mafunzo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe Mzumbe ni kuwasaidia wataalamu wa ununuzi, ugavi na usafirishaji waweze kufata hatua zinazotakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo kutoka chuo Kikuu Mzumbe kampasi kuu Morogoro, Mhadhili Dkt. Paul Nsimbiwa Kabelele, amesema kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuwasaidia wataalam hao kujua utaratibu wa kuingia makubaliano kuanzia hatua ya awali mpaka miktaba ya manunuzi inapofanyika.
“Mafunzo haya yatachangia kupunguza changamoto katika kusimamia miktaba kwani tumekuwa tukishindwa kupata thamani ya manunuzi na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali” amesema Dkt. Nsimbiwa.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa wanaamini elimu watakayopata kwa muda wa siku tatu katika Chuo Kikuu Mzumbe itawasaidia katika kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi.
Chuo Kikuu Mzumbe kimedhamiria kuendelea kutoa mafunzo kwa wataalam wa ugavi, ununuzi na usafirishaji katika nyanja mbalimbali ili kuhakikisha ubora na ufanisi katika sekta hii.