Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Yanga SC wamekutana na kipigo cha mabao 3 -1 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa leo Novemba 7, 2024 katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko Tabora United walikuwa wanaongoza mabao 2- 0 ambayo yakifungwa na nyota mzawa Offen Francis Chikola katika dakika ya 19 na 45+ 4.
Kipindi Cha pili Tabora United walipata bao la tatu lililofungwa na Kiungo Mkongo Nelson Omba Munganga dakika ya 78 akimalizia pasi ya mshambuliaji mzawa Ibrahim Ahmada.
Bao la kufutia machozi kwa Yangu lilifungwa na Kiungo mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 90+5 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo.
Kwa ushindi huo Tabora United anafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusongea hadi nafasi ya 6, wakati Yanga inabaki na pointi 24 nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Simba SC baada ya wote kucheza michezo 10.