Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha Hezron Mbise akizungumza katika mahafali hayo mkoani Arusha .
Mkurugenzi wa shule ya Naurey Golden Soils Stephen Ndossy akizungumza na wazazi pamoja na mwanafunzi katika mahafali hayo.
…………
Happy Lazaro, Arusha .
Arusha .Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha Hezron Mbise amewaomba wazazi kurudi nyuma na kuwatupia jicho la pili kwa watoto wa kiume kwa kuwa ndio Taifa la kesho kwani wamesahaulika sana.
Aidha amesema kuwa, hivi sasa nguvu nyingi zimeelekezwa katika kuangalia watoto wa kike tu huku watoto wa kiume wakiwa wameachwa nyuma sana kitendo ambacho amewataka kuwekeza nguvu zaidi kwa watoto wa kiume pia.
Mbise ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya wahitimu wa kidato che nne wa shule ya sekondari Naurey Golden Soils iliyopo kata ya Nkoanrua wilayani Arumeru mkoani Arusha ,mahafali yaliyoenda sambamba na harambee ya kukamilisha jengo la ghorofa ya shule hiyo.
Aidha amesema kuwa, watoto wa kiume nao wanahitaji ulinzi mkubwa sana kwani hivi sasa kumekuwepo kwa vitendo vingi sana vya ukiukwaji wa maadili hivyo namna tunavyowekeza wa watoto wa kike na kwa watoto wa kiume iwe hivyo pia.
“Nampongeza sana Mkurugenzi Mkurugenzi shule hii kwa namna ambavyo anapambana kutoa elimu iliyo bora na ya vitendo kwa wanafunzi wetu ambayo mwisho wa siku itawasaidia sana kuweza kujiajiri na kutengeneza ajira.”amesema Mbise.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule ya Naurey Golden Soils Stephen Ndossy amesema kuwa,shule hiyo kitaaluma imekuwa ikifanya vizuri sana na hiyo ni kutokana na kuwa na walimu.mahiri katika utoaji wa elimu kwa njia jumuishi kwa wanafunzi .
Ndossy amefafanua kuwa, ufaulu katika mitihani ya Taifa ya kidato.cha pili kwa miaka miwili iliyopita ulikuwa mzuri sana hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilikuwa mpya ambapo kwa mwaka 2022/23 walikuwa na watahiniwa 28 na kati ya hao watahiniwa 17 wakipata daraja la kwanza na watahiniwa 11 walipata faraja la pili.
Ndossy amesema kuwa,while hiyo imekuwa na ushirikiano wa kimataifa na shirika la TES School in Afrika lililopo nchini Denmark ambao wamekuwa wakiwawezesha misaada mbalimbali hasa Samani shule na vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano ( Tehama).
Ameongeza kuwa, shirika hilo limewasaidia kupata kanisani wengine kutoka nchini kwao wanazotoa ufadhili wa ada ya shule kwa baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka familia zisizo na uwezo wa kutosha kiuchumi ambapo jumla ya wanafunzi nane wamenufaika na msaada huo.
Amesema kuwa,katika swala la uwajibikaji kwa jamii shule hiyo amesema kuwa shule hiyo.imekuwa ikiwajibika kwa jamii ya halmashauri ya wilaya ya Meru hasa katika.tarafa ya Poli na kata zake ambapo kwa mwaka 2022 waliweza kuratibu upatikanaji wa Samani za shule za msingi za Moivaro na Ambureni pamoja na shule ya sekondari Poli ambapo ufadhili huo.ulikuwa wa jumla ya shs 50 milioni.
Amesema kuwa, mpango huu wa ushirikiano kati ya TES School in Africa na shule hiyo ni mpango endelevu ambao unalenga kuzisaidia shule nyingi zaidi za wilaya ya Arumeru.
Naye Mkuu wa shule hiyo , Tito Kaaya akisoma hotuba amesema kuwa wanafunzi hao wamefanikiwa kufanya vizuri kitaaluma na kimaadili na kiroho ambapo kwa miaka miwili mfululizo katika mitihani ya kidato cha pili wanafunzi wamekuwa wakifanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Kaaya amesema kuwa,wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.ikiwemo uhaba wa nyumba,ambapo changamoto nyingine ni wazazi wa kiume kutowajibika ipasavyo katika swala la malezi kwa kutojihusisha na hali za watoto wao wawapo shuleni kwani wanawaachia jukumu hilo wanawake tu jambo ambalo ni changamoto kubwa.
Aidha amewaomba wazazi pande zote mbili kuhakikisha wanawajibika katika swala zima la malezi ya watoto wao kwani kila mzazi ana mtizamo wake na nafasi yake katika malezi.