Na Mwandishi wetu, Simanjiro
GLISTEN Pre & Primary School ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeendelea kuongoza kwa ufaulu katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba.
Shule ya Glisten kupitia Mkurugenzi wake Justin Nyari mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani na mfanyabiashara maarufu wa jijini Arusha, imekuwa na matokeo chanya kila wakati.
Kwa matokeo ya darasa la saba kwa mwaka huu wa 2024, kwenye wilaya ya Simanjiro, Glisten imeongoza kwa kupata ufaulu wa asilimia 100 alama A, wastani wa 268.5556.
Shule ya Notre Dame Osotwa imekuwa ya pili kwa ufaulu wa asilimia 100 alama A wastani wa 256.5333, shule ya St. Augustine imepata ufaulu wa asilimia 100 daraja A wastani wa 253.3462 na New Light Pre & Primary imepata ufaulu wa asilimia 100 daraja A wastani wa 252.8333.
Shule nyingine ni New Vision iliyopata ufaulu wa asilimia 100 alama B wastani wa 238.1875, shule ya Al- Fallah imepata ufaulu wa asilimia 100 alama B wastani wa 230.8182.
Shule msingi ya Tumaini imepata ufaulu wa asilimia 100 alama B wastani wa 200.8750, shule ya msingi Kazamoto imepata ufaulu wa asilimia 100 alama B wastani wa 196.7105.
Shule ya msingi Losokonoi kijiji alichozaliwa mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka, imepata ufaulu wa asilimia 100 alama B wastani wa 193.1000 na shule ya Engata imekuwa kwenye 10 bora kwa ufaulu wa asilimia 100 alama B na wastaniwa 188.4167.