Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam AZAM FC inakuwa timu ya kwanza kukomba pointi tatu mbele ya Mabingwa watetezi Yanga kwenye mchezo wa ligi msimu wa 2024/25.
Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, baada ya dakika 90 ubao umesoma Yanga 0-1 Azam FC bao la ushindi likifungwa na Sillah dakika ya 33.
Katika mchezo wa leo Yanga ilikosa huduma ya beki Bacca dakika ya 21 ambaye alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo huo na kadi 8 za njano zimetolewa.
Miongoni mwa nyota ambao wameonyeshwa kadi za njano kwa upande wa Azam FC ni kiungo Feisal Salum, Mtasigwa, huku kipa Mustapha yeye akioneshwa kadi ya njano kwa kile kilichotafsriwa kuwa alikuwa anapoteza muda.
Ikumbukwe kwamba Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi mapema alibainisha kuwa walikwama kupata maandalizi mazuri kutokana na mechi ngumu ambazo walicheza ugenini.