Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion) kuhusu Kilimo barani Afrika, katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususan waliopo kwenye sekta ya kilimo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya majadiliano (round tables discussion) na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ikiwemo Viongozi wa Serikali ya Marekani, wamiliki wa makampuni binafsi pamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGOs) leo tarehe 31 Oktoba 2024, mjini Iowa, Marekani. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya kilimo zinazopatikana Tanzania na namna Tanzania inavyoweza kunufaika kupitia wawekezaji hao.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia mjadala kuhusu Kilimo Barani Afrika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani kando ya mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation tarehe 30 Oktoba, 2024.