Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu na Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani, Bw. Julian Banzi Raphael akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya uongozi wa kimkakati yaliyofanyika kwenye chuo cha Benki Kuu Mwanza Leo Oktoba 28, 2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu na Naibu Gavana, Utawala na Udhibiti wa Ndani, Bw. Julian Banzi Raphael, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uongozi wa kimkakati yaliyofanyika katika Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu, Prof. Tadeo Satta na Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu, Dkt. Nicas Yabu.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu, Prof. Tadeo Satta akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya uongozi wa kimkakati yaliyofanyika kwenye chuo cha Benki Kuu Mwanza Leo Oktoba 28, 2024.
Mkuu wa Chuo cha Benki Kuu, Dkt. Nicas Yabu akizungumza katika ufunguzi huo wa wa mafunzo ya uongozi wa kimkakati yaliyofanyika kwenye chuo cha Benki Kuu Mwanza Leo Oktoba 28, 2024.
Mtoa Mada kutoka Chuo cha Bandari, Dr. Lufunyo Hussein, akifafanua jambo kuhusu Uongozi wa Kimkakati wakati wa mafunzo kwa viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania, Burundi, Ghana, Zimbabwe na Zambia; benki za biashara na taasisi za fedha nchini, yanayofanyika katika Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza.
Mtoa Mada kutoka Benki Kuu ya Zambia, Ms. Mumbi Mwila, akielezea jambo kuhusu Uongozi wa Kimkakati wakati wa mafunzo kwa viongozi wa Benki Kuu ya Tanzania, Burundi, Ghana, Zimbabwe na Zambia; benki za biashara na taasisi za fedha nchini, yanayofanyika katika Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza.
Viongozi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Burundi, Ghana, Zimbabwe na Zambia; benki za biashara na taasisi za fedha nchini, wakifuatilia mada katika mafunzo ya uongozi wa kimkakati yaliyofanyika katika Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza.
…………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo ya Uongozi wa Kimkakati kwa viongozi wa taasisi mbalimbali za kifedha ili waweze kuziongoza taasisi zao kwa umahili mzuri.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Benki Kuu Mwanza yakiwa na jumla ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Benki Kuu Mwanza, Profesa Tadeo Satta amesema mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Benki za Biashara za hapa nchini,BoT,Benki Kuu ya Ghana,Benki Kuu ya Zambia,Benki Kuu ya Zimbabwe,na Benki Kuu ya Burundi ambapo aliongeza kuwa hao ni washirika wao wanaoshirikiana katika kubadilishana usoefu, mawazona utaalamu na namna ya kuendesha sekta za fedha katika nchi zao.
Amesema taasisi za fedha zinahitaji uongozi madhubuti kwenye sekta ya fedha ili waweze kusapoti ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Bila kuwa na viongozi ambao wana weledi wakimkakati ufikiwaji wa malengo hayo unakuwa ni changamoto ndio maana tunatoa mafunzo ili sekta ya fedha iweze kutekeleza majukumu yake vizuri kwani sekta hii ni muhimu kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote”, alisema Profesa Satta
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Tusekelege Joune amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongoza taasisi zao kwa weledi sanjari na kuwathamini wafanyakazi wao hatua itakayosaidia kuongeza ufanisi wa kazi utakaowezesha Benki kupata faida.
Awali akifungua mafunzo hayo Naibu Gavana,Utawala na Udhibiti wa Ndani kutoka BoT, Julian Raphael aliwasihi washiriki kuyatumia mafunzo hayo katika kutekeleza majukumu yao ili yaweze kuleta tija kwa jamii.