…………………
Na Sixmund Begashe – Dodoma.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) leo tarehe 28 Oktoba 2024 Jijini Dodoma, imekutana na Watumishi 23 wa ajira mpya kundi la pili na kuwakabidhi barua za ajira na barua za kupangiwa vituo vya kazi kwenye Wizara hiyo.
Akizungumza na watumishi hao wapya Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Raslimaliwatu Bw. Bernad Marcelline amesema kuwa ajira hizo mpya ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuendelea kufungua milango ya ajira kwa watanzania wenye sifa.
Aidha, Bw. Marcelline licha ya kuwapongeza kwa kupata fursa hiyo ya ajira amewataka kwenda kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia maadili ya Utumishi wa umma kwa maslahi mapana ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Taifa kwa ujumla.