Na Mwandishi wetu, Simanjiro
CHAMA cha kulinda na kutetea haki za walimu Tanzania CHAKUHAWATA Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kinasikitika kutangaza kifo cha mwalimu wa shule ya msingi Terrat Yusuph Maiko Sambura.
Katibu wa CHAKUHAWATA Wilaya ya Simanjiro, Costantine Joachim Tunch amesema mwalimu Sambura amefariki kifo cha kawaida akiwa kwenye kituo chake cha kazi.
“Kwa masikitiko makubwa CHAKUHAWATA Wilaya ya Simanjiro tunasikitika kuondokewa na mwanachama wetu mwalimu mwenzetu kutoka shule ya msingi Terrat,” amesema mwalimu Tunch.
Amesema uongozi wa CHAKUHAWATA ngazi ya wilaya wanatoa pole na wamewasilisha salamu za rambirambi ya shilingi laki 2 kwa familia ya marehemu.
“Mazishi yanafanyika Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma Oktoba 27 na tunamuombea mwalimu mwenzetu apumzike kwa amani,” amesema mwalimu Tunch.
Amewaasa walimu wengine kujiunga na CHAKUHAWATA kwani kinalinda na kutetea ipasavyo haki za walimu nchini.
“Hata makato yetu ni rafiki kwani huwa inatolewa shilingi elfu tano pekee kwa mwezi tofauti na vyama vingine,” amesema mwalimu Tunch.