Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Slaa (Mb) akiwa amekata utepe kuashiria uzinduzi wa Zahanati ya kijiji cha Igonia kilichopo katika Wilaya ya Mkalama, Mkoani Singida.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Slaa (Mb) akiwa akipiga makofi mara baada ya kukata utepe katika uzinduzi wa Zahanati ya kijiji cha Igonia kilichopo katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.
Wananchi kijiji cha Igonia wakipiga makofi mara baada ya kuzinduliwa kwa Zahanati ya kijiji hicho m kilichopo katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.
Waziri Slaa akiwa na Watumishi wa Zahanati ya Kijiji cha Igonia wilayani Mkalama.
Waziri Slaa akiwa katika zahanati ya Igonia wlayani Mkalama.
………..
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa (Mb) amezindua Zahanati ya kijiji cha Igonia kilichopo katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida iliyoaanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2013 na baadae Serikali kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 80.
Zahanati hiyo ambayo imeanza kufanya kazi mpaka sasa imehudumia wakazi 880 tangu ilipoanza kufanya kazi mwezi wa sita ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kijiji hicho kina idadi ya wakazi 1408.
Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho Waziri Silaa amesema Zahanati hiyo imejibu kiu changamoto ya wananchi waliyokuwa wakikumbana nayo kwa kufuata huduma za afya kwa zaidi ya kilomita 10.
Amesema zahanati hiyo inavifaa vya kisasa ambavyo vitasaidia kuwahudumia wananchi wa eneo bila kutembea umbali mrefu kwenda katika maeneo mengine kufuata huduma.
Aidha ametoa wito kwa wakazi hao kuisimamia zahanati hiyo ili iendelee kutoa huduma bora.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amewahakikishia wananchi kuwa serikali itasimamia zahanati hiyo ili kuboresha huduma zake kwa wananchi.