Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Amemzawadia Kiasi cha Shilingi Milioni 50 Mwimbaji wa Muziki wa zamani Mzee Steve Hiza aliyeimba wimbo wa Tanzania ndiyo nchi ya Furaha.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa Hafla ya Tuzo za Muziki Tanzania ambapo amesema Mhe Rais ametoa zawadi hiyo Mahususi kwa Mzee Hiza kutokana na mchango wake kwenye Muziki.
“Tanzania yetu ndio nchi ya kusifiwa, kote ulimwenguni watu wote wanajua, Tanzania yetu ndio nchi ya furaha” ni moja ya kionjo cha Wimbo huo mkongwe ambao ni maarufu midomoni mwa watu umeimbwa na Mzee Steve Hiza.