Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, leo imepokea msaada wa mifuko 150 ya saruji kutoka kwa wanachama wa New MZRH SACCOS ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kwa mwaka huu, msaada unaolenga kusaidia ujenzi wa vyumba vya upasuaji unaoendelea kwaajili ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa New MZRH SACCOS alisisitiza umuhimu wa kutoa misaada kwa jamii na kueleza kwamba kila mwaka wanajitahidi kufanikisha miradi mbalimbali ya kijamii. “niutaratibu wetu tuliojiekea kama SACCOS kila mwaka na kwa leo tumeona tutoe mifuko 150 ya saruji kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa hospitali yetu,
Nduu Nsenye ameeleza kuwa, Wananchama wa NEW MZRH SACCOS wanaamini katika kutoa msaada kwa jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya 6 ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za afya nchini.
Nae Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, akikabidhiwa mifuko hiyo na kuishukuru New MZRH SACCOS kwa msaada wao mkubwa. Dkt. Mbwanji alisema,
“Msaada huu utaleta mabadiliko makubwa katika huduma zetu. Tunawakaribisha wadau wote kuungana nasi katika juhudi hizi za kuboresha huduma za afya.”
“lengo la kuanzishwa kwa SACCOS ilikuwa ni kuwasaidia watumishi ili waweze kupata mikopo kwa masharti nafuu kwa kutumia SACCOS, lakini sasa tunaona matunda, hawajaishia kujikopesha wao, ila wamekuja sasa kusaidia na kuunga mkono juhudi za Serikali, kwahiyo tunawapongeza sana na tunaendelea kuwahamasisha watumishi wote kuendelea kuwa wanancha walio hai na wale ambao hajajiunga tunawahamasisha nao wajiunge – Dkt. Mbwanji.
Vilevile Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Dkt. Dino Mwaja amewashukuru Wananchama wao kwa moyo wao wa kujitolea na kueleza kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka ili kuwezesha kazi ya ujenzi kuendelea na kueleza kuwa msaada huo wa saruji ni hatua muhimu katika kuhakikisha hospitali inakamilisha ujenzi wa vyumba vya theater, ambayo ni sehemu muhimu katika kutoa huduma bora za afya kwa wagojwa. Wananchi wa Mbeya sasa wanatarajia huduma bora zaidi za afya kupitia miradi hii inayoendelea.