Wakazi wa kata ya Nyatwali Wilayani Bunda Mkoani Mara wameanza kuondoka kupisha maeneo yao baada ya serikali kulipa fidia ili kupisha eneo hilo kwaajili ya Upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na mapitio yawanyama.
Wakazi hao takribani 4112 wa mitaa Minne ya Tamau, Nyatwali,kariakoo pamoja na Serengeti tayari 2888 wameshalipwa huku waliobaki niwale ambao hawajafanyiwa Tathimini ya makaburi.
Tayari Serengeti imetenga kulipa kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 45 kulipa wakazi hao ikiwaa ni awamu ya Kwanza ya zoezi hilo
Akizungumza Kamishina msaidizi wa uhifadhi Mathew Mombo anayeshulikia maswala ya Migogoro na Mipaka hifadhi zote Tanzania Alisema Serikali umeamua kulitwaa eneo hilo kutokana na umhimu wake katika kwa masilahi mhimu ya Taifa huku akipongeza ungwana uliofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wakazi hao.
” Tunampongeza DKT Samia kufanya maaamuzi magumu ili kuwalipa wakazi hawa kutokana eneo hilo kuwa na umhimu mkubwa Sana Kwaajili ya ikolojia ya serengeti.
Mombo amesema watu waliobaki kulipwa kwa sasa imebaki idadi ndogo ambapo Alisema niwa wenye makaburi na wengine ambao fidia hawakufanyiwa Tathimini.