Na Sophia Kingimali.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imezindua ofisi mpya kwa ajili ya kuwahudumia walipa kodi binafsi wa hadhi ya juu lengo ni kuwahudumia kulingana na hadhi yao ili kuchochoa ulipaji kodi wa hiyari lakini pia kuhakikisha hao walipa kodi wanapata huduma hiyo kulingana na hadhi yao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo iliyopo Jengo la Golden Tower Posta jijini Dar es salaam Kamishna mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema ofisi hiyo itahudumia walipa kodi wa hiyari ambao wanahadhi ya hali juu.
Amesema ofisi itatoa huduma kwa makundi manne ambao ni wamiliki wa makampuni ambao mauzo yake yanazidi milioni 20 kwa mwaka,wamiliki binafsi wa hisa zenye thamani ya biilioni 2.5,wenye ubia wa makampuni ambao zinazidi bilioni 20 kwa mwaka,lakini pia viongozi wa mihimili mitatu ya nchi.
“Tumewalenga wao tunataka tuwape huduma kwanza makampuni yao yenyewe yanatulipa kodi wafanyakazi wanatulipa kodi hao sisi kwetu ni wa hadhi ya juu”,Amesema Mwenda.
Ameongeza kuwa Watu hao ambao ni wa hadhi ya juu pamoja ya makampuni na wafanyakazi wao kulipa kodi lakini nao wanamapato yao binafsi ambayo ni lazima alipe kodi.
Amesema kwa kuanza wameanza na walipa kodi 158 ambapo walipa kodi binafsi wapo 111 na viongozi ambao watakuja baadae watakua 47.
Amesema mchango wao ni mkubwa na ndio maana wameona kuna haja ya kuwawekea utaratibu na kuwapa huduma bora kwani kushindwa kuwawekea mazingira bora serikali itashindwa kukusanya mapato.
“Hawa watu walikuwa wakilipa lakini tumewawekea mazingira mazuri ili tuweze kuwafuatilia na kuwashauri vizuri na kulipa kodi wanayostahiri”,Amesema.