Na Neema Mtuka
Rukwa
Mkurugenzi wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Kanda ya nyanda za juu kusini Magharibi Mhandisi Sotco Nombo amewataka Wananchi kutumia jiko janja ili kutunza mazingira.
Mhandisi Nombo amesema hayo wakati wa tukio la kuangaza maisha ya winfrida Nyami mkazi wa Kijiji Cha Kaengesa ambaye anaishi na ulemavu kwa kumuunganishia umeme bila malipo.
Nombo alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi zao za kuunga mkono kampeni ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya nishati safi ya kupikia na kuboresha maisha ya wananchi.
Alifafanua kuwa kitendo Cha kumuunganishia umeme Winfrida na kumpatia jiko janja la kupikia ni shukrani kwa Jamii inayotumia nishati ya umeme na kujiinua kiuchumi.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki katika tukio hilo akiwemo Luwis Miemba amelitaka shirika la umeme Tanzania TANESCO kuendelea kutoa huduma stahiki kwa kuwafikishia umeme katika makazi yao.
Tukio hilo limefanyika katika hafla fupi ya kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo Tanesco imejipambanua kwa vitendo katika kuwasaidia wananchi na kuunga mkono jitihada za Rais Samia kuhusu nishati safi ya kupikia.