Na WAF, TABORA
Madakatari Bingwa wa Rais Samia kwa ushirikiano na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete wamefanikiwa kuokoa uhai wa mama wa watoto 11 mwenye umri wa miaka 40 tu.
Kwa mujibu wa wataalam inasemekana mama huyo alifika Hospitali ya wilaya ya Kaliua akiwa hajitambua na akiwa na ujauzito wa mtoto wa 12 haliniliyosababisha wampe rufaa.
“Ilinilazimu kwenda Hospitali baada yakuona natokwa na damu nyingi kwenye via vya uzazi lakini watoto wangu wote 11 nilikuwa najifumgulia nyumbani bila tatizo” amesema Bi Situ Hamis mkaazi wa Kaliua mkoani Tabora.
Akiongea hospitalini hapo Dkt. Gregson Kabata wa Hospitali ya Kitete alisema walimpokea mama huyo akiwa hajitambui na kumfikishia chumba cha uangalizi maalum
“Ni kweli tulimpokea Bi Situ akitokea Hospitali ya Wilaya ya Kaliua akiwa kwenye hali mbaya ikatulazimu kumfanyia matibabu ya haraka akiwa chini ya uangakuzi wa wauguzi na madaktari kwa kudra za mungu ndio afya yake imeimarika hivi” amesema Dkt. Kabata.
Kwa upande wake mratibu wa zoezi hilo kwa mkoa wa Tabora kutola Wizara ya Afya Dkt. Eveline Maziku, ameendelea kuwahimiza wanawake kote nchini nchini kuzingatia maelezo na miongozo inayowataka wanawake wajawazito kwenda kituo cha afya pindi anapojitabua ni mjamzito na kuhudhuria mpaka wakati wakujifungu awe ameenda mara saba.
Kambi ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia wamekuwa mkoani Tabora kunzia Oktoba 07 hadi 12, 2024 kwa ajili ya huduma za kibingwa na kuwajengea uwezo watumishi ngazi ya msingi.