Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mheshimiwa Said Mshana, amemwakilisha Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof Makame Mbarawa katika kikao cha Nchi Wanachama wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor) kilichofanyika jijini Kinshasa nchini DRC.
Kikao hicho pamoja na masuala mengine, kuliikaribisha Zambia kuwa Mwanachama Mpya wa Ushoroba wa Kati.
Zambia inakuwa mwanachama wa Saba wa Ushoroba wa Kati baada ya kusaini Mkataba wa CCTTFA tarehe 8 Oktoba,2025 katika tukio lililofanyika jijini Kinshasa