Mchungaji wa kanisa la Enendeni church for All Nations kutoka jijini Dar es Saalam ,Mchungaji Christian Saley akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
…….
Happy Lazaro, Arusha .

Wadau mbalimbali mkoani Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha la uzinduzi wa kitabu cha Ubatizo na aina  zake utakaofanyika katika kanisa la Elim Pentekoste Unga Ltd   oktoba 6  mwaka huu.

Hayo yamesemwa  mkoani Arusha na   Mchungaji wa kanisa la Enendeni church for All Nations kutoka jijini Dar es Saalam ,Mchungaji Christian Saley wakati akizungumza  na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na maandalizi ya  tamasha hilo.
Mchungaji  Saley amesema kuwa, lengo la uzinduzi wa  kitabu hicho ni.ili kuelimisha watu kuhusu maana halisi ya Ubatizo kwani eneo hilo limekuwa likisumbua watu wengi  sana .
“Kitabu hiki kitazinduliwa na Askofu  mkuu wa  Elim Pentekoste  jimbo la Arusha ,Askofu Philipo Fisoo  ambapo wageni rasmi watakuwa wawili ambao ni Hellena na Clara ambao kwa pamoja watashirikiana katika uzinduzi huo.”amesema.
 Amesema kuwa kitabu hicho kitawawezesha  watu kujua maana ya Ubatizo halisi wa kibiblia ambao Mungu anautambua .
Mchungaji Saley amesema kuwa,tamasha hill litahudhuriwa na waimbaji mbalimbali ,hivyo kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kumuunga  mkono katika tamasha hilo ambalo litakuwa  la aina yake .