Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingireza ya St.Pius iliyopo mkoani Arusha,Pius Kimati akizungumza katika mahafali.hayo.mkoani Arusha
Diwani wa kata ya Oldonyosambu,Raymond Lairumbe akizungumza katika.mahafali hayo.
Naye Mkuu wa shule hiyo , Ernest Lembris akizungumza kuhusiana na shule.
……..
Happy Lazaro,Arusha .
Wazazi wametakiwa kujitambua na kutenga muda wa kukaa na watoto wao badala ya kuwa bize na shughuli za maisha kutokana na hali ilivyo sasa hivi ya kuporomoka kwa maadili kwa kiwango kikubwa.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkurugenzi wa shule ya mchepuo wa kiingireza ya St.Pius iliyopo mkoani Arusha,Pius Kimati wakati.akizunguza katika mahafali ya 8 ya darasa la saba shuleni hapo .
Kimati amesema kuwa, wazazi wengi wamesahau majukumu yao ya familia kutokana na kuwa bize na shughuli za maisha jambo ambalo.linachangia kuendelea kuporomoka kwa maadili kutokana na kuwaachia watoto wao uhuru .
“Wazazi mnapowaachia watoto wenu uhuru badala ya kuwafuatilia ndio mnachangia kuendelea kuporomoka kwa maadili kwani watoto wanakuwa na uhuru kupita kiasi na hawana watu wa kuwakemea kuhusu matukio hayo.”amesema .
Aidha amesema kuwa ,shule hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa watoto kuhusu swala la maadili ambayo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na vitendo mbalimbali na kuweza kuwa mabalozi wazuri katika.maeneo yao.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Oldonyosambu,Raymond Lairumbe amewataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa kuhakikisha wanapunguza matumizi mabaya ya simu kwani wengi wao hutumia simu tofauti na inavyotakiwa.
Raymond amesema kuwa,ni wajibu wa wazazi kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri ya nyumbani kwa ajili.ya watoto wao badala ya kukimbizana na shughuli za kijamii ambazo zinawafanya kuwa bize na kusahau majukumu yao.
“Sasa hivi kuna janga kubwa sana la ushoga nawaomba sana wazazi wakae pamoja na watoto waoñbbbbbb kwa karibu na kuzungumzia swala hilo wala wasione aibu kuzungumza nao kwani tunapoelekea sasa hivi ni pabaya sana endapo wazazi tusipochukua hatua za haraka.”amesema.
Naye Mkuu wa shule hiyo , Ernest Lembris amesema kuwa ,shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma katika matokeo ya darasa la nne mfululizo na darasa la saba na hiyo ni kutokana na elimu.bora inayotolewa na walimu .
Amesema kuwa, wamekuwa wakifundisha wanafunzi hao stadi za kazi na kuweza kujitegemea pindi wanapohitimu badala ya kukaa mtaani tu .
Aidha baadhi ya wanafunzi waliohitimu masomo yao walisema kuwa wanashukuru shule hiyo kwa namna ambavyo imeweza kuwaandaa kujiajiri kwa kuwa na elimu ya kubuni vitu mbalimbali.