……….
Happy Lazaro, Arusha .
Wazazi wa wanafunzi wa kidato cha nne na kidato cha pili wanaosoma katika shule ya sekondari ya wavulana Tengeru Boys iliyopo mkoani Arusha wamechanga kiasi cha shs 64 milioni kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa mitihani ambapo kiasi cha shs 1.344 bilioni kinahitajika kwa ajili ya kukamilisha jengo hilo.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mkuu wa shule ya wavulana Tengeru boys, Gaudence Mtui wakati akizungumza katika mahafali ya 17 ya wavulana Tengeru boys ambapo jumla ya wanafunzi 136 walihitimu yakiwemo mahafali ya 4 ya Holy Ghost viziwi.
Mtui amesema kuwa mbali na wazazi hao kuchangia fedha hizo , Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imewachangia kiasi cha shs 15 milioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo ambapo linatarajia kuanza hivi karibuni na litaweza kuhudumia wanafunzi mia mbili kwa wakati mmoja na kuondoa changamoto wakati wa kufanya mitihani.
“Jengo tulilokuwa tukitumia ni dogo kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi iliyopo sasa hivi hivyo kukamilika kwa ujenzi huo utasaidia sana wanafunzi hao kuweza kutumia jengo hilo kwa ajili ya mitihani ambapo ukumbi huo utakuwa na ofisi nne na madarasa sita.”amesema .
Aidha amewataka wadau mbalimbali kusaidia juhudi hizo zilizoanzishwa na wazazi kwani wameonyesha mfano wa kuigwa kwa ajili ya kusaidia watoto wao kuwa na ukumbi huo .
Mtui amesema kuwa ,kumekuwepo kwa kiwango.kikubwa cha ufaulu shuleni hapo ambapo mitihani ya Mock na CSSC ambayo walifanya kikanda vijana wote walishika nafasi ya kwanza katika kanda ya kaskazini Magharibi inayojumisha mikoa ya Kulima,Arusha na Manyara.
Ameongeza kuwa,kwa upande wa shule ya Holy ghost viziwi walimu wanajitahidi sana wakiamini kuwa ulemavu sio kizuizi cha kufikia ndoto ya mafanikio kwa vijana wetu wasiosikia, ambapo wahitimu wamekuwa wakipata daraja la kwanza mpaka daraja la tatu na vijana wote waliomaliza kidato cha nne kati.ya 2021,2022,na 2023 walifanikiwa kuendelea na masomo katika ngazi zingine za kitaaluma kama kidato cha tano na vyuo vya kati.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika.mahafali hayo Dk.Mariamu Kobelo amesema kuwa , shule hiyo imekuwa ikiwalea watoto na kuwafundisha malezi mazuri ya kiroho sambamba na kuwafundisha kuhusu swala zima la maadili na kuweza kuepukana na vitendo viovu hususani wanapokuwa mtaani.
Amesema kuwa, kila mmoja anashuhudia namna ya ambavyo kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili unaosababishwa utandawazi ,hivyo nawaomba wazazi wajitahidi kuwa karibu na watoto wao kwani ndio kwanza safari ya maisha imeanza .
“Nawaomba sana wazazi mhakikishe mnawajengea watoto mazingira mazuri ya elimu.kwani elimu.ndio urithi pekee unaoweza kumpatia mtoto kwa ajili ya maisha yake ya baadaye”amesema Mariamu.
Nao baadhi ya wanafunzi waliohitimu masomo yao,Anthony Mushi na Abiri Rembo wamesema kuwa shule hiyo imewaandaa kuweza kujiajiri kutokana na kufundishwa masomo mbalimbali.kwa vitendo zaidi na kuweza kujifunza maswala mbalimbali ambayo yatawasaidia kwa maisha yao ya baadaye ikiwemo kuweza kuanzisha biashara mbalimbali.