RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Rais) Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mradi wa Fumba Port Zanzibar Awadh Twalib Ali, michoro ya majengo inayotarajiwa kujengwa katika Bandari ya Mkoani Pemba, wakati wa Uzinduzi wa Meli ya Kwanza ya Makontena na Makabidhiano ya Bandari ya Mkoani, hafla hiyo iliyofanyika leo 30-9-2024.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuzindua Meli ya Kwanza ya Makontena ya Lamu Shipping Limited, ikiwa katika Bandari ya Mkoani Pemba ikishusha Makontena, wakati wa hafla ya Uzinduzi huo wa Meli ya Makontena ya Kwanza na Makabidhiano ya Bandari ya Mkoani kwa Kampuni ya Fumba Port kwa ajili ya uendeshaji wa Bandari hiyo, hafla hiyo iliyofanyika leo 30-9-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Kampuni ya Fumba Port, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Akif Ali Khamis, akitowa maelezo wakati wa Uzinduzi wa Meli ya Kwanza ya Makontena ya Lamu Shipping Limited, ikiwa katika Bandari ya Mkoani Pemba na kushusha Makontena ya Wafanyabiashara wa Pemba, uzinduzi huo uliofanyika leo 30-9-2024.(Picha na Ikulu)