Na Prisca Libaga , Arusha
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imesema kuwa, itaendelea kudhamini mchezo wa mpira wa magongo, maarufu Golf, ambao una heshima kubwa Ulimwenguni ili uweze kuchezwa na watu wengi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Ahadi hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa biashara wa Airtel makao makuu Joseph Muhere kwenye ufunguzi wa mashindano hayo ya kila mwezi yanayofanyika kwenye uwanja wa Golf Jijini Arusha ambayo yanashirikisha wachezaji 60
Amesema kuwa kampuni ya Airtel imejitosa kudhamini mpira huo kwa kushirikiana na Club ya Arusha ya Gyhmkana, ili ufahamike zaidi kama ulivyo mpira wa miguu uweze kuchezwa na watu wengi zaidi.
Muhere, amesema kuwaudhamini huo ni mwanzo wajitihada za kukuza mchezo huo ili kuwavutia Vijana wengi waweze kushiriki na kuucheza ambapo kupitia mpira huo wachezaji watapata fursa ya kukutana na Kampuni zingine na wafadhili mbalimbali ambapo watapata fursa ya kujadiliana kuhusu biashara na uchumi .
Amesema kuwa mchezo huo sio wa matajiri kama unavyoonekana bali ni mchezo wa watu wote hivyo wananchi watoe woga wajitokeze kushiriki kucheza kwa kuwa ni mchezo kama mchezo mingine.
Upande wake Meneja wa mashindano hayo ya mpira wa magongo,wa Club ya Arusha Golf, Abbas Larji,
ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kudhamini mashindano hayo yanayofanyika kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mzima .
Ameziomba kampuni zingine na wadau wengine kujitokeza kudhamini mchezo huo wa mpira wa golf au magongo,ambao unachezwa na watu wote wanawake wanaume na Vijana.
Mdhamini wa Arusha Gyhmkhana Club, Paulo Matthysen, amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika kila mwezi yana faida kubwa ikiwemo kujiweka sawa kimwili
Hivyo akawashauri wazazi kuwahamasisha Vijana wao wakashiriki kucheza mchezo huo ambao kila mwezi kutakuwepo na mashindano ambayo yamedhaminiwa na Kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Airtel.
Ameshauri Vijana wengi kuhamasika kucheza mpira huo kama ilivyo kwa Vijana wengi wa Lugalo, Jijini Dar es Salaam,kuna Vijana wengi wanaoshiriki kucheza mpira huo ili uenee maeneo mbalimbali.
Amesema kuwa kuna idadi kubwa ya Wanawake kutoka mkoani Arusha ambao wanacheza mpira huo nje ya nchi na kuleta heshima kwa taifa.