Klabu ya Simba imepokea wageni maalum na wanafamilia wa mpira kutoka nchini Italia, tukio ambalo limeleta hisia za heshima na undugu ndani ya klabu hiyo maarufu ya Tanzania.
Wageni hao ni Emilliano Lisi, Branca Luigi, na Daniela Ciapetti, wote wakiwa na historia ya kipekee katika soka la Italia.
Emilliano Lisi ni mchezaji wa zamani wa AS Roma, klabu maarufu nchini Italia, ambapo alicheza nafasi ya beki wa kati (RCB) na pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Italia.
Kuwepo kwa Emilliano Lisi, ambaye ameweka alama kubwa kwenye ulimwengu wa soka, kumeleta furaha kwa wadau wa Simba, hasa kutokana na mchango wake katika historia ya mpira wa miguu wa kimataifa.
Ingawa hawajatajwa sana kwenye medani ya umaarufu wa soka, wana uhusiano na historia ya michezo nchini Italia, na uwepo wao umepokelewa kwa heshima kubwa.
Wageni hawa walipokelewa rasmi kabla ya mchezo wa Mzizima Derby kuanza kati ya Simba SC na Azam FC , tukio lililofanyika katika Uwanja wa New Aman Complex, visiwani Zanzibar. Walikabidhiwa jezi za Simba na wajumbe wa bodi ya klabu hiyo , akiwemo Dkt. Seif Muba na Ndugu Crescentius Magori, kwa niaba ya klabu hiyo.
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Simba.